Mada ya Kwanza
KUANDINDA BARUA
Kuna barua ya kirafiki na barua rasmi na barua pepe
Barua ya kirafiki
Hii inaandikiwa kwa ndugu, wazazi rafiki au mpenzi.
Inaitwa barua ya kirafiki/barua ya kindugu au barua ya kimapenzi
Kuna vipengele vya barua ya kirafki (there are different parts of a friendly letter)
1. Anwani ya mwandishi (address of the sender)
2. Tarehe (date)
3. Mwanzo wa barua – jina la anayeandikiwa (name of the receiver)
Ndugu: brother, sister, relative, closer than just a friend.
Mpendwa mama, Mama Mpendwa, Mama: Dear mother.
Mpendwa Baba, Baba mpendwa,
Dada, Rafiki, Mwalimu, Yohana, n.k. Mpenzi Anna, Juma‐ hutumika kwa wapenzi, au
bwana na bibi.
4. Salamu/maamkio (greetings)
5. Sehemu kuu (main body)
6. Hitimisho (conclusion)
Kuna njia nyingi za kumaliza/kukamilisha barua, kwa mfano:
i. Wasalaam
ii. Ni mimi, …..
iii. Kakako, ….
iv. Kakako mpendwa, ….
v. Wako, ….
vi. Akupendaye…
vii. Anayekukumbuka…
viii. Rafiki wa kufa na kupona…
7. Sahihi au saini au jina lako
Mfano wa kwanza
Shule ya Sekondari Nyanungu,
S.L.P 145
Tarime
22/03/2002
Baba Mpendwa,
Salaam sana. Natumaini umzima pamoja na jamaa na marafiki wa hapo kijijini. Nami ni
mzima na ninaendelea na masomo yangu vizuri hapa shuleni.
Napenda kukujulisha kuwa maendeleo yangu ya masomo hapa shuleni ni mazuri sana. Katika
mtihani wa kumaliza mwaka wa pili nimeshika nafasi ya pili kati ya wanafunzi 195 wa
kidato cha tatu. Nimeamua kusomea mchepuo wa masomo ya Biashara ili hatimaye niwe
mchumi wa nchi yetu. Hivyo, naomba tuzidi kuombeana heri.
Pamoja na mafanikio hayo yote, kuna tatizo kubwa sana ambalo linazidi kuniandamana hapa
shuleni. Tatitizo hili linanikosesha kabisa raha. Kila wakati huwa ninahuzunika. Tatizo hili
huwa la umaskini. Sina hata shilingi tano ya kukununulia kipande cha mhogo. Hivyo naomba
uuze yule jogoo mkubwa unitumie pesa haraka iwezekanavyo.
Wasalimie wote wanaonifahamu hapo kijijini. Msalimie sana shangazi yangu Ekeraya Moka
Abarisi
Wako akupendaye
Inyumba Endegwa
24 Chamberlain Road,
Sanduku La Posta 1843,
Graniteside,
Harare
09 Desemba 2023
Mpendwa ….
Habari yako rafiki ….. ? Mimi sijambo. Ninaamini na wewe pia hujambo.
Ninakuandikia barua hii kukuambia kuhusu likizo yangu ya Victoria Falls. Nilienda
tarehe…….. Nilienda na ……… Tulisafiri kwa…….. Tulipofika, tuliishi …… na pia
tulikula ……. Siku ya kwanza tuliona wanyama kama……
Tuliona pia maporomoko ya Victoria. Ni mazuri sana rafiki yangu. Siku ya pili tulienda
kuogelea. Siku ya tatu tuliondoka na kurudi nyumbani kwetu.
Kwa kweli nilifurahia likizo yangu ya Victoria Falls. Ninaamini tutaonana mwaka huyu
rafiki yangu.
Wako
Enock
Mada ya Pili
Kupika ughali/ Cooking sadza
Vifaa/ Utensils and ingedients
1. Sufuria
2. Mwiko
3. Maji
4. Unga wa mahindi
5. Jiko au moto
Hatua
1. Washa jiko/moto
2. Weka maji kwenye sufuria halafu weka sufuria jikoni
3. Acha maji yachemke
4. Tengeneza mchanganyiko wa unga wa mahindi na maji mpaka uwe uji
5. Acha uji uchemke
6. Baada ya dakika chache, ongeza unga na uchanganye vizuri hadi iwe ngumu na kuiva
7. Ipukua upakue
Msamiati/ Vocabulary
Washa turn on
Weka put
Acha let/leave
Yachemke to boil
Tengeneza prepare
Mchanganyiko mixture
Mpaka till
Uji porridge
Baada after
Dakika minutes
Chache few
Ongeza add
Hadi until
Ngumu hard
Ipua remove from (stove/fire)
Pakua serve
MADA YA TATU
SWAHILI TIME
Time in Kiswahili refers to 12 hours of day time and 12 hours of night time. 7:00 am is
referred to as saa moja asubuhi to mean that it is the first hour of the day. 7:00 pm is called
saa moja usiku to indicate that it is the first hour of the night.
Vocabulary
English Swahili Time Swahili
6:00 a.m. 12:00 in the morning Saa Kumi na mbili asubuhi
7:00 a.m. 1:00 in the morning Saa moja asubuhi
8:00 a.m. 2:00 in the morning Saa mbili asubuhi
9:00 a.m. 3:00 in the morning Saa tatu asubuhi
10:00 a.m. 4:00 in the morning Saa nne asubuhi
11:00 a.m. 5:00 in the morning Saa tano asubuhi
12:00 p.m. (Noon) 6:00 in the afternoon Saa sita alasiri
1:00 p.m. 7:00 in the afternoon Saa saba alasiri
2:00 p.m. 8:00 in the afternoon Saa nane alasiri
3:00 p.m. 9:00 in the afternoon Saa tisa alasiri
4:00 p.m. 10:00 in the evening Saa kumi jioni
5:00 p.m. 11:00 in the evening Saa kumi na moja jioni
Saa kumi na mbili jioni /
6:00 p.m. 12:00 in the evening
Thenashara
7:00 p.m. 1:00 in the evening Saa moja jioni
8:00 p.m. 2:00 in the night Saa mbili usiku
9:00 p.m. 3:00 in the night Saa tatu usiku
10:00 p.m. 4:00 in the night Saa nne usiku
11:00 p.m. 5:00 in the night Saa tano usiku
12:00 a.m. (Midnight) 6:00 in the night Saa sita usiku
1:00 a.m. 7:00 in the night Saa saba usiku
2:00 a.m. 8:00 in the night Saa nane usiku
3:00 a.m. 9:00 in the night Saa tisa usiku
4:00 a.m. 10:00 in the morning Saa kumi asubuhi
5:00 a.m. 11:00 in the morning Saa kumi na moja asubuhi
English Swahili
Morning Asubuhi
Daytime Mchana
Afternoon Alasiri
Evening Jioni
Night Usiku
Minute Dakika
Half Nusu
Time Saa
Quarter to Kasorobo
English Swahili
Quarter past na robo
Less Kasoro
English Swahili
9:45 Saa nne kasorobo
11:30 Saa tano unusu / Saa tano na nusu
10:15 Saa nne na robo
12:15 Saa sita na dakika kumi na tano
8:20 Saa mbili na dakika ishirini
7:40 Saa moja na dakika arobaini / Saa mbili kasoro dakika ishirini
6:50 Saa kumi na mbili na dakika hamsini / Saa moja kasoro dakika kumi